Jumapili, 3 Mei 2015

Ni amri zipi muhimu alizousiwa mtume s.a.w na mola wake s.w, nasi ni muhimu kuzichunga katika dini yetu

Ni amri zipi muhimu alizousiwa mtume s.a.w na mola wake s.w, nasi ni muhimu kuzichunga katika dini yetu

 


        JAWABU

 Amri ya kwanza kuteremshiwa mtume s.a.w na ALLAAH S.W ni kusoma.
Akaambiwa :
(بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ)
[Surat Al-Alaq 1 ]

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,

Amri ya pili Akaambiwa Asimame usiku kufanya ibada kwa ajili ya ALLAAH S.W,
(قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا)
[Surat Al-Muzzammil 2]

Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!

 Amri ya tatu ni kusoma qurani kwa utaratibu wake kama alivyosomeshwa na mwalimu wake Jibriil a.s

(أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا)
[Surat Al-Muzzammil 4]

na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo.

 Amri ya tatu ni Kusimama na kuwahofisha watu wake wa karibu  kutokana na adhabu ya ALLAAH ikiwa hawakufuata njia ya haki,

(وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ)
[Surat Ash-Shu'ara 214]

Na uwaonye jamaa  walio karibu nawe.

Na akaamrishwa afikishe yale yote aliyoteremshiwa na ALLAAH S.W,  wala asifiche kitu
(يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ ۖ وَإِنْ لَمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ)
[Surat Al-Maeda 67]

Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.

Na akaamrishwa asubiri kama walivyosubiri mitume wengine kabla yake.

(فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ وَلَا تَسْتَعْجِلْ لَهُمْ ۚ كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَ مَا يُوعَدُونَ لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِنْ نَهَارٍ ۚ بَلَاغٌ ۚ فَهَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الْفَاسِقُونَ)
[Surat Al-Ahqaf 35]

Basi subiri, kama walivyo subiri Mitume wenye stahmala kubwa, wala usiwafanyie haraka. Siku watakayo yaona waliyo ahidiwa itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa moja ya mchana. Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine isipo kuwa walio waovu tu?

Awe ni mwenye kumsabbih

na kuswali  ALLAAH S.W,

(فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُنْ مِنَ السَّاجِدِينَ)
[Surat Al-Hijr 98]

فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُنْ مِنَ السَّاجِدِينَ

Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia.

Kudumisha ibada mpaka yamfike mauti.
(وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ)
[Surat Al-Hijr 99]

 Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.

 Ndugu zangu :
Haya yote hayawezi kutimia mpaka ipatikane amri ya kwanza kutekelezwa.
Nayo ni amri ya "IQRA'A "

 Na kusoma huko hakuwezi kuwa na faida yoyote mpaka iwe ni kusoma kwa ajili ya ALLAAH na kwa kutaka msaada wake kama alivyosema yeye mwenyewe ALLAAH S.W katika amri hiyo ya mwanzo.

 Elimu yenye ubora ni yenye kuhifadhi sifa ya umoja wa umma bora.

 Ni lazima tufahamu kuwa kuna tofauti kubwa kati ya;

"Bora elimu "

        Na

"Elimu bora "

 Msomi bora ni bora kuliko bora msomi.

 Elimu ya kukufurisha waumini si elimu bora.

Elimu bora ni kuwafanya waumini wawe katika Imani na Amani.

 Tunamuomba ALLAAH S.W ELIMU yenye manufaa na manufaa ya elimu.

ALLAAHU AALAMU.

 ELIMU KWANZA.

Jumapili, 16 Februari 2014

AYA YA SIKU

JE! HUONI YA KWAMBA ALLAH HUYASUKUMA MAWINGU, KISHA HUYAAMBATISHA, KISHA HUYAFANYA MIRUNDI? BASI UTAONA MVUA IKITOKA KATI YAKE. NA HUTEREMSHA KUTOKA JUU KUTOKA KWENYE MILIMA YA MAWINGU MVUA YA MAWE, AKAMSIBU NAYO AMTAKAYE NA AKAMUEPUSHA NAYO AMTAKAYE. HUKURUBIA MMETUKO WA UMEME WAKE KUPOFUA MACHO”. [24:43]

Ijumaa, 13 Septemba 2013

TUMIA SIMU YAKO YA MKONONI KURUSHA MATUKIO LIVE

ULIMWENGU WA TEKNOLOJIA

vipi unaweza kutumia simu yako ya mkononi kwa kurusha tukio la live,angalia hiyo video hapo chini na bila shaka utafaidika.

Jumatano, 4 Septemba 2013

NANI YUPO TAYARI KUJIWEKEA KINGA YA KILA SIKU?!

JE UNATAKA KINGA YA KWELI?!


عن عثمان بن عفان رضي الله عنه قال: قالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: 

"مَا مِنْ عَبْدٍ يَقُولُ في صَبَاحِ كُلّ يَوْمٍ وَمَسَاءِ كُلّ لَيْلَةٍ:

بِسْمِ الله الّذِي لا يَضُرّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ في الأرْضِ وَلا في السّمَاءِ وَهُوَ السّمِيعُ العَلِيمُ،

ثَلاَثَ مَرّاتٍ إلَّا لم يضُرّهُ شَيْءٌ". 

AMESEMA MTUME S.A.W
MJA YEYETO ATAKAESEMA KILA SIKU ASUBUHI NA KILA SIKU JIONI,"KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU AMBAE KWA KUMTAJA JINA LAKE HAKUNA MADHARA YOYOTE YATAKAYO NIPATA 
,ARDHINI WALA MBIGUNI,HAKIKA YEYE NDIO MSIKIZI MJUZI 
MARA TATU HATOPATWA NA MADHARA YOYOTE
HADITHI HII IMEPOKELEWA NA IBN MAAJAH NO:5089
HILO NENO LA KULISEMA MARA TATU KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI AMBALO NDIO LITAKUWA KINGA YAKO NI:
BISMILLAHI LA YADHURRU MAA SMIHI SHAY-U FIL-ARDHI WALA FI SSAMAI WAHUWA SSAMIIU L ALIIM
NANI YUPO TAYARI KUJIWEKEA KINGA YA BURE KILA SIKU BILA MALIPO YOYOTE??!! IKARIRINI HIYO MUTAONA FAIDA YAKE

Jumapili, 1 Septemba 2013

soma kisa hiki ni kizuri sana:


MAPENZI YA KWELI NI VITENDO WALA SI MANENO

waliishi mume na mke katika hali ya umasikini sana,jioni moja mke alimwambia mumewe:naomba uninunulie kitana ili nichanie nywele zangu,zipendeze!!!
mume alimwangalia kwa jicho la huzuni sana,akwambia:sinauwezo huo kwani saa yangu inataka mkanda ili niivae mpaka leo nimeshindwa kuinunulia!
mwanamke hakumjibu mbovu ila alitabasamu.
siku ya pili baada ya mume kutoka kazini kwake,alikwenda sokoni na kuiuza saa yake kwa bei ndogo sana,na akanunua kitana alichoagizwa na mke wake,lakini aliporudi nyumbani akamkuta mke wake kakata nywele zake na zimekuwa ndogo sana kiasi kwamba hazitaki kitana!!
kila mmoja alimwangalia mwenzake huku machozi yakiwatoka si kwa lolote isipokuwa kila mmoja anampenda mwenzake na analinda kutimiza mahitaji yake kwa njia yoyote ile!!
KUMBUKA DAIMA:
JITAHIDI KATIKA KUMFURAHISHA UNAEM
PENDA(MKE/MUME/WAZAZI/NDUGU...)KWA NJIA ZOTE HATA KAMA NJIA YA KUFIKIA LENGO HILO NI NGUMU,KWANI MAPENZI YA KWELI NI VITENDO WALA SIO MANENO MDOMONI

VIPI UNAWEZA KUTENGENEZA PICHA ZAKO ONLINE?!

darsa hii kwa video inatuelekeza namna ya kutengeneza picha online huku zikiwa na mtazamo mzuri kabisa na maumbile ya vitu mbali mbali kama carrot gari na.........angalia hiyo video utafaidika inshaallah


KISA HICHI NAKUSHAURI UKISOME!
MZEE ANA MIAKA 80!!!
KUNA SIKU ALIRUDI KUTOKA MSIKITINI,AKAGONGA MLANGO WA NYUMBA YAKE,HAKUFUNGULIWA MPAKA AKAZIMIA!!
BAADA YA MDA KIDOGO,MKE WAKE AKAJIULIZA MBONA MUME WANGU KACHELEWA?!
AKATOKA KUMUANGALIA......AKAMKUTA KAZIMIA CHINI YA MLANGO,AKAPATWA NA HOFU,AKAMWAGIA MAJI KIDOGO YA USO,AKAAMKA,MKE AKAMWOMBA SAMAHANI SANA KWA KUCHELEWA KWAKE KUMFUNGULIA!!!
SIKILIZA NINI YULE MZEE ALIMJIBU MKEWE!!!
ALIMWAMBIA:WALLAH!! SIKUZIMIA KWA AJILI YA MCHOKO AU KWA KUWA UMECHELEWA SANA KUNIFUNGULIA!!!
LAKINI WAKATI HUO NILIKUMBUKA SIKU NITAKAYOSIMAMA KWA MOLA WANGU,NA IKAFUNGWA MILANGO YA PEPO MBELE YANGU(SIKURUHUSIWA KUINGIA PEPONI).
NILIZIMIA KWA HOFU YA SIKU HIYO!!--SUBHANNA LLAH--
EWE MOLA WETU TUNAKUOMBA MWISHO MWEMA YA RAB,NA TUNAKUOMBA TUINGIE PEPONI PAMOJA NA MANABII WAKO NA WALIOKUAMINI NA WALIOKUFA KATIKA KUIPIGANIA DINI YAKO!