Jumapili, 3 Mei 2015

Ni amri zipi muhimu alizousiwa mtume s.a.w na mola wake s.w, nasi ni muhimu kuzichunga katika dini yetu

Ni amri zipi muhimu alizousiwa mtume s.a.w na mola wake s.w, nasi ni muhimu kuzichunga katika dini yetu

 


        JAWABU

 Amri ya kwanza kuteremshiwa mtume s.a.w na ALLAAH S.W ni kusoma.
Akaambiwa :
(بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ)
[Surat Al-Alaq 1 ]

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,

Amri ya pili Akaambiwa Asimame usiku kufanya ibada kwa ajili ya ALLAAH S.W,
(قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا)
[Surat Al-Muzzammil 2]

Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!

 Amri ya tatu ni kusoma qurani kwa utaratibu wake kama alivyosomeshwa na mwalimu wake Jibriil a.s

(أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا)
[Surat Al-Muzzammil 4]

na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo.

 Amri ya tatu ni Kusimama na kuwahofisha watu wake wa karibu  kutokana na adhabu ya ALLAAH ikiwa hawakufuata njia ya haki,

(وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ)
[Surat Ash-Shu'ara 214]

Na uwaonye jamaa  walio karibu nawe.

Na akaamrishwa afikishe yale yote aliyoteremshiwa na ALLAAH S.W,  wala asifiche kitu
(يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ ۖ وَإِنْ لَمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ)
[Surat Al-Maeda 67]

Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.

Na akaamrishwa asubiri kama walivyosubiri mitume wengine kabla yake.

(فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ وَلَا تَسْتَعْجِلْ لَهُمْ ۚ كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَ مَا يُوعَدُونَ لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِنْ نَهَارٍ ۚ بَلَاغٌ ۚ فَهَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الْفَاسِقُونَ)
[Surat Al-Ahqaf 35]

Basi subiri, kama walivyo subiri Mitume wenye stahmala kubwa, wala usiwafanyie haraka. Siku watakayo yaona waliyo ahidiwa itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa moja ya mchana. Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine isipo kuwa walio waovu tu?

Awe ni mwenye kumsabbih

na kuswali  ALLAAH S.W,

(فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُنْ مِنَ السَّاجِدِينَ)
[Surat Al-Hijr 98]

فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُنْ مِنَ السَّاجِدِينَ

Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia.

Kudumisha ibada mpaka yamfike mauti.
(وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ)
[Surat Al-Hijr 99]

 Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.

 Ndugu zangu :
Haya yote hayawezi kutimia mpaka ipatikane amri ya kwanza kutekelezwa.
Nayo ni amri ya "IQRA'A "

 Na kusoma huko hakuwezi kuwa na faida yoyote mpaka iwe ni kusoma kwa ajili ya ALLAAH na kwa kutaka msaada wake kama alivyosema yeye mwenyewe ALLAAH S.W katika amri hiyo ya mwanzo.

 Elimu yenye ubora ni yenye kuhifadhi sifa ya umoja wa umma bora.

 Ni lazima tufahamu kuwa kuna tofauti kubwa kati ya;

"Bora elimu "

        Na

"Elimu bora "

 Msomi bora ni bora kuliko bora msomi.

 Elimu ya kukufurisha waumini si elimu bora.

Elimu bora ni kuwafanya waumini wawe katika Imani na Amani.

 Tunamuomba ALLAAH S.W ELIMU yenye manufaa na manufaa ya elimu.

ALLAAHU AALAMU.

 ELIMU KWANZA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni